Shirika la CHRISTIAN AID kwa ushirikiano na idara ya afya kaunti ya mombasa pamoja na wadau mbali mbali limetoa hamasa kwa jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hasa ya virusi vya korona likitoa tahadhari kwa jamii hususan kwa zile ambazo zinapuuza umuhimu wa chanjo kwa kisingizio kuwa korona imepitwa na wakati.
Kwenye mazungumzo na vyombo vya habari baada ya kuandaa hafla ya kutoa mafunzo kuhusu umuhimu wa chanjo kwa wadau mbali mbali ikiwemo viongozi wa kidini, shirika la vijana Pamoja na wadau wa afya, afisa mkuu wa shirika hilo ADBDUL AGUKO ameonyesha kughadhabishwa na hatua ya jamii kudinda kuchukua chanjo jambo ambalo limechangia dozi za chanjo kuharibika.
Aguko kadhalika amesema kuwa kuna hofu kwamba iwapo jamii haitachukua swala la chanjo kwa uzito basi uchumi wa taifa uko katika hatari ya kudidimia.
Kwa upande wa wadau wa afya wakiongozwa na dr Maryam Mwajumla amewahimiza wanajamii kujitokeza kwa wingi kupokea chanjo ili wuweze kudhibiti kabisa msambao wa korona akipuzilia kauli kwamba korona imepitwa na wakati .
Aidha Amani Katana ambaye ni mwakilishi wa vijana kadhalika amewahimiza vijana kupokea na kuubiri injili ya chanjo huku akisema kuwa kama vijana watahakikisha kuwa ujumbe utafikia jamii kupitia mdahalo kule mashinani.
BY DAVID OTIENO