Jumla ya wakaazi 1800 kutoka vijiji 16 vya eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale wamepokea chakula cha msaada kilichotolewa na serikali ya kitaifa katika eneo hilo.
Kulingana na naibu kamishna wa Msambweni Kipkoech Lotiatia, chakula hicho kimetolewa kwa wakaazi wasiojiweza baada ya kuathirika na janga la ukame.
Akizungumza wakati wa ugavi wa chakula hicho, Lotiatia amesema kuwa walengwa wamepokea mchele, maharagwe na nyama za mikebe.
Kwa upande wao baadhi ya wakaazi waliopokea chakula hicho wameipongeza serikali kuu kwa kuwakumbuka wakati huu wa kiangazi.
Wakiongozwa na Jimmy Charo, wakaazi hao wameitaka serikali kuongeza chakula hicho ili kiwafikie waathiriwa zaidi.
BY EDITORIAL DESK