HabariNews

Wakfu wa Aga Khan unatekeleza mradi ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwao.

Wakfu wa Aga Khan unatekeleza mradi wa miaka miwili wa kutoa mafunzo ya kibiashara kwa vijana unaofadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwao.

Mshirikishi wa mradi huo Stella Wambua amesema kuwa mafunzo hayo yalianzishwa kufuatia mchipuko wa janga la corona uliopelekea kusambaratika kwa biashara nyingi nchini.

Akizungumza kwenye maonyesho ya kibiashara yaliyofanyika katika eneo la Diani kaunti ya Kwale, Wambua amedokeza kwamba wanalenga kutoa mkopo wa kufadhili biashara bunifu kwa vijana 60 kutoka kaunti za Kwale, Mombasa, Kilifi na Lamu.

Kwa upande wao vijana wa kaunti hiyo walioshiriki kwenye maonyesho hayo wameelezea matumaini ya kupata ufadhili huo ili kukuza biashara zao.

Wakiongozwa na Abdulkarim Mwinyi, vijana hao wameupongeza wakfu huo kwa kuwapa mafunzo hayo ili kuzikabili changamoto za biashara yao.

BY EDITORIAL DESK