Kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Mombasa amabae ni mwakilishi wa wadi ya likoni Athman mwamiri, amesema kuwa bunge hilo litahakikisha kuwa madeni yaliyosawa kisheria yatalipwa chini ya utalawa wa sasa baada ya uchunguzi wa kina.
Akizungumza na vyombo vya habari katika makao ya bunge baada ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa wengi Mwamiri amesema kuwa kila mwanakandarasi aliyetumikia watu wa Mombasa kihalali ni sharti atalipwa ili kupunguza madeni yanayokumba seriklai ya kaunti hiyo.
Kadhalika kiongozi huyo amesisitiza kwamba kama bunge litashirikiana kwa ukaribu mkubwa na serikali ya kaunti hiyo kuhakikisha kuwa wananchi wanatapa walichoahidiwa wakati wa kampeni huku akiongeza kwamba kwa sasa wako katika harakati ya kukutuna na majopo kazi ambayo yaliundwa na gavana kuangazia swala la afya na fedha ndani ya kaunti hiyo.
Wakati hu huo Mwamiri amewataka wawakilishi wadi kushiriki katika vikao vya bunge ili kupunguza swala la kutowajibika na badae kubwagia lawana serikali .
BY EDITORIAL DESK