HabariNews

CHUO KIKUU CHA KENYA METHODIST TAWI LA MOMBASA KIMEAJIANDAA VYA KUTOSHA KUTEKELEZA MFUMO WA ELIMU YA UMILISI CBC.

Mkurugenzi wa chuo kikuu cha Kenya Methodist tawi la Mombasa Dr. Winfred Githinji amesema chuo hicho kimeajiandaa vya kutosha kutekeleza mfumo wa elimu ya umilisi CBC.

Akizungumza wakati wa hafla ya mwigo wa kufuzu mahafala wa chuo hicho, Dr Githinji amedokeza kuwa tayari chuo hicho kimebuni kamati inayoshughulikia utekelezaji wa mfumo wa CBC chuoni humo.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mfumo huo wa CBC utahakikisha taasisi za elimu nchini zinaendana na mahitaji ya elimu ulimwenguni.

Kuhusu hafla ya mwigo wa kufuzu mahafala wa chuo hicho, mkurugenzi huyo amesema wamekuwa wakifanya hafla ya mwigo ili kutoa fursa kwa wanafunzi wenye matatizo ya usafiri hadi mako makuu ya chuo hicho kwa hafla kamili.

BY EDITORIAL DESK