HabariNewsSiasa

Gavana wa jimbo la Kwale atoa onyo kali dhidi ya wafanyikazi wa umma wasiowajibika.

Onyo kali limetolewa na gavana wa jimbo la Kwale dhidi ya wafanyikazi wa umma katika serikali ya kaunti ya hiyo akisema wale wote wasiowajibika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Akizungumza huko Eshu eneo wadi ya Ramisi Achani amesema kumekuwa na tetesi kuhusu utepetevu miongoni mwa wahudumu wa afya wanaodaiwa kuwanyanyasa wagonjwa.

Aidha Achani amekariri kwamba ni jukumu la kila mfanyikazi wa serikali ya kaunti kuwajibikia kazi yake.

Wakati uo huo amewataka viongozi mbali mbali wa Kaunti ya Kwale wakiwemo Wawakilishi wadi washirikiane na serikali ili kufanikisha ajenda za maendeleo.

Kauli yake hiyo imeungwa mkono na Mwakilishi Wadi wa Ramisi aliye pia Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kaunti ya Kwale Hanifa Badi Mwajirani aliyeahidi kushirikiana na uongozi wa Serikali ya Kaunti ya Kwale kikamilifu, akisema siasa zilikwisha baada ya uchaguzi.

BY EDITORIAL DESK