HabariNews

KNUT imeitaka serikali kupitia mamlaka ya kudhibiti kampuni za bima nchini (IRA) kuimarisha huduma za bima ya afya ya walimu.

Chama cha walimu nchini (KNUT) kimeitaka serikali kupitia mamlaka ya kudhibiti kampuni za bima nchini (IRA) kuimarisha huduma za bima ya afya ya walimu.

Katibu wa chama hicho Kaunti ya Kwale Bashir Kilalo amedai kwamba bima hiyo inawakandamiza walimu hasa wanapotafuta huduma za matibabu.

Akizungumza katika warsha ya kutoa mafunzo kwa walimu kuhusu bima, Kilalo amelalamikia utoaji wa huduma duni kupitia bima ya matibabu ya walimu.

Kwa upande wake afisa wa mamlaka ya IRA Evans Kibagendi amesema kwamba tayari wameanzisha mpango wa kutoa mafunzo kwa walimu kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto za bima.

Kibagendi amedokeza kuwa mpango huo unalenga kuwahamasisha viongozi wa vyama vya walimu nchini kuhusu umuhimu wa kuekeza katika bima.

BY EDITORIAL DESK