HabariNews

Wakaazi waeneo la Kisauni watakiwa kushirikiana na maafisa wa usalama.

Idara ya usalama usalama kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano na viongozi wa kisiasa eneo la Kisauni imewataka wakazi eneo hilo kushirikiana kikamilifu na maafisa wa usalama ili kudhibiti ukosefu wa usalama unaoshuhdiwa mara kwa mara eneo hilo.

Kwenye mazungumzo na vyombo vya habari baada ya mkutano wa dharura wa kujadili usalama eneo hilo, naibu kaunti komishna wa kisauni Jamlick Mbuba amewataka wananchi kuwa wepesi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili kurahisisha zoezi la kukabiliana na wahalifu eneo hilo.

Mbuba aidha amewataka wakazi kutohofia kutoa Ushahidi mahakamani dhidi ya wahalifu ili kusaidia katika kuwafungilia mashatka washukiwa.

Kwa upande wake mbunge wa eneo hilo Rashid Bedzimba ametoa onyo kwa wazazi ambao wanawalinda Watoto wanaoshiriki uhalifu akitaja kuwa watakaopatikana wataadhibiwa kishheria.

Aidha Mwakilishi wadi eneo hilo Morgan Matsaki ameeleza matumaini yake ya kumalizwa kwa uhalifu eneo hilo akidai kuwa umechangia kudororesha uchumi kwa kiwango kikubwa.

Mkutano huo unajiri maasaa machache tu baada ya mtu mmoja kukatwa mapanga usiku wa kuamkia leo eneo la mtopanga wiki moja tu baada ya watu watatu kuvamiwa na kkuachwa na majeraha ya mapanga huko huko mtopanga.

BY DAVID OTIENO