HabariMombasaNews

Madereva wa texi kaunti ya Mombasa wanasema wanakadiria hasara kutokana na mgomo wa marubani.

Madereva wa texi kaunti ya Mombasa wanasema wanakadiria hasara kutokana na mgomo wa marubani wa shirika la ndege la Kenya air ways unaoendelea nchini.

Kulingana na Madereva hao mgomo wa marubani unaathiri pakubwa mapato yao ya kila siku.

Wakizungiumza na mezayetu ya habari madereva hao wamedokeza kuwa biashara yao ilikuwa imeanza kupata afueni baada ya janga la korona.

Wanasema iwapo mgomo huo ambao umeingia siku ya nne hii leo utaendela huenda ukawarejesha nyuma kibiashara.

Aidha madereva hao wamesema wateja waliokuwa tegemeo lao la kila siku kuwasafirisha sasa wamebaki njia panda hali ambayo imepunguza idadi ya wateja.

Sasa wamezitaka idara husika kushuglikia mgomo huo.

BY EDITORIAL DESK