Afisa wa mamlaka ya kudhibiti kampuni za bima nchini (IRA) Evans Kibagendi amesema kuwa fedha hizo zimekusanywa tangu kuanzishwa kwa hazina hiyo mwaka wa 2005.
Akizungumza katika eneo la Matuga kaunti ya Kwale, Kibagendi amedokeza kwamba hazina hiyo inalenga kuwafidia wakenya walioekeza kwenye kampuni hizo.
Kwa upande wake mmoja wa wahudumu wa sekta ya uchukuzi kaunti hiyo David Wanyoike amelalamikia kucheleweshwa kwa malipo yao na kampuni za bima.
Aidha, Wanyoike ameitaka serikali kuwapiga msasa maajenti wa bima ili kukabiliana na visa vya ulaghai dhidi ya wakenya.
BY EDITORIAL TEAM