HabariNews

Wahudumu wa mabaa kutoka kaunti ya Kwale wamelalamikia hatua ya baadhi ya benki za humu nchini ya kuwanyima mikopo ya kuendeleza biashara zao.

Mwenyekiti wa wahudumu hao Richard Onsongo ameilaumu pakubwa benki ya ABSA kwa madai ya kuwanyima fedha za mikopo.

Akizungumza katika hoteli moja eneo la Diani, Onsongo ameitaka benki hiyo kuwapa mikopo licha ya kutokuwa na leseni za biashara zao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa wateja katika benki ya ABSA nchini Peter Mutua amekanusha madai hayo akisema kuwa benki hiyo inatoa mikopo kwa kila mfanyibiashara.

Mutua amedokeza kwamba tayari wanaendeleza mpango wa kutoa hamasa kwa wananchi kuhusu jinsi ya kupata fedha hizo.

BY NEWS DESK