HabariNews

Wavuvi watano kutoka eneo la shimoni huko lungalunga kaunti ya kwale wanazuiliwa nchini Somalia.

Wavuvi watano kutoka eneo la shimoni huko lungalunga kaunti ya kwale wanazuiliwa nchini Somalia katika mji WA mudoa Kwa majuma mawili sasa.

Wavuvi hao ambao wamezuiliwa na polisi nchini kutokana na kutoelewana na muajiri wao anayedai kulipwa fidia ya shilingi laki moja kabla ya kuwaruhusu kurudi nyumbani.

Wakiongozwa na Mohamed Omari Mgala akizungumza kupitia njia ya simu Mgala amesema kuwa wanaishi katika mazingira magumu tangu kukamatwa Kwao na kuitaka serikali kufanya Hali ili kuwarejesha nyumbani salama.

Miongoni waliozuiliwa ni pamoja na omari she,Hamisi zito,Kimosha Abdallah na Abdallah Gwashe.

Wavuvi hao walikua miongoni mwa wavuvi 12 waliofululiza Hadi nchini Somalia kuendeleza shughuli za uvuvi kupitia usimamiza WA mfanyibiashara mmoja maarufu kutoka kaunti ya lamu.

Ukosefu WA usalama nchini Somalia na vitisho kutoka Kwa wanamgambo WA alshabab ukawa chanzo cha kuvunjwa Kwa mkataba baina yao na mwajiri wao,aliyewalazimu kulipwa gharama za kuwaleta Somalia kabla ya kuwaruhusu kurudi nyumbani.

Hata 7 Kati ya wavuvi 12 wamerejea nyumbani huku 5 wakiendelea kuzuiliwa Somalia Hadi pale watakapolipa shilingi laki moja gharama ya mwajiri.

BY EDITORIAL TEAM