HabariNews

Asilimia 80 ya ajali za barabarani zinazotokea humu nchini zimetajwa kusababishwa na wahudumu wa sekta ya bodaboda.

Asilimia 80 ya ajali za barabarani zinazotokea humu nchini zimetajwa kusababishwa na wahudumu wa sekta ya bodaboda.

Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa taasisi ya wahandisi nchini Munga Mungatana anayesema kuwa ajali hizo zinatokana na ukosefu wa mafunzo ya sheria za barabarani miongoni mwa wahudumu hao.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya waaathiriwa wa ajali duniani iliyofanyika eneo la Ukunda, mkurugenzi wa bodi ya wahandisi nchini Roselina Jilo amesisitiza haja ya waendeshaji wa pikipiki kupewa mafunzo hayo ili kuzuia visa vya ajali.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda kaunti ya Kwale Nehemiah Kinywa amedokeza kwamba jumla ya visa 40 vya ajali za bodaboda ziliripotiwa mwaka uliopita.

Kinywa ameeleza kuwa visa hivyo vinazidi kuongezeka hasa tunapoelekea kwa msimu wa krismasi kutokana na idadi kubwa ya wahudumu wasiokuwa na leseni za kuendesha pikipiki.

BY NEWS DESK