Taasisi ya wahandisi nchini (IEK) imewaonya wakenya dhidi ya wahandisi bandia kufuatia kukithiri kwa visa vya majumba yanayojengwa kuporomoka.
Rais wa taasisi hiyo Eric Ohaga amewataka wamiliki wa majumba kuwaajiri wahandisi waliohitimu katika ujenzi wa nyumba.
Akizungumza katika kongamano la 29 lililowaleta pamoja zaidi ya wahandisi elfu 3 katika eneo la Diani kaunti ya Kwale, Ohaga amesema kwamba hatua hiyo itasaidia kukabiliana na ongezeko la visa hivyo.
Kwa upande wake mbunge wa Ragwe kutoka kaunti ya Homa bay Lilian Gogo amesema kuwa visa hivyo vitadhibitiwa endapo sheria za ujenzi zitatekelezwa.
Gogo ameeleza kuwa sheria zilizopo hazijatekelezwa kikamilifu, hali inayochangia kuongezeka kwa visa vya majumba yanayoporomoka nchini.
BY EDITORIAL TEAM