Viongozi wa kidini kaunti ya Kwale wametaja Baadhi ya Wazazi kama waliochangia katika ongezeko la visa vya migogoro ya kindoa hususan kwa wanandoa wachanga hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa ongezeko la talaka.
Wakiongozwa na sheikh Amani Hamisi, wamesema baadhi ya wazazi wamekua wakiwalazimisha watoto wao kuingia katika ndoa kutokana na sababu zao tofauti tofauti pasi na vijana hao kujipanga kisaikolojia.
Kiongozi huyo wa kidini amewahimiza viongozi wengine wa kidini kushirikiana ili kuhakikisha vijana wanapitia mafunzo yatakayowatayarisha kisaikolojia kabla ya kuingia katika ndoa.
BY EDITORIAL DESK