HabariNews

Wanajamii wa kaunti ya kwale watakiwa kuripoti visa vya mimba za mapema.

Shirika la sauti ya wanawake tawi la kaunti ya Kwale limetaja mbinu mpya zinazotumiwa na baadhi ya wanajamii ili kutoripoti visa vya mimba za mapema kaunti ya Kwale kama zitakazochochea kuongezeka kwa visa hivyo zaidi iwapo hazitasitishwa.

Mwenyekiti wa shirika hilo kaunti hiyo Mwanakombo Jerumani, amesema kunashuhudiwa visa vya baadhi ya wakaazi wa Kwale wanaosafiri katika hospitali za kaunti jirani ikiwemo Mombasa kupata huduma za afya kwa waathiriwa wa mimba za mapema.

Mwanakombo amesema kulingana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa vitengo mbalimbali katika jamii ikiwemo kutoka kwa wakunga, zinaonyesha wazi kukithiri kwa mimba za mapema katika jamii.

Hata hivyo amesema wazazi wanajukumu kubwa la kushirikiana katika malezi bora kwa watoto ili kuwakinga na dhulma za kijinsia ikiwemo mimba za mapema pamoja na ulawiti.

BY EDITORIAL DESK