Baraza la magavana na wizara ya afya sasa italazimika kuunda jopo maalum litakaloangazia mpito wa wahudumu wa afya wanaohudumu chini ya mkataba mfupi wa miaka 3 kabla ya mkataba huo kukamilika mwaka ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraza hilo ambaye pia ni gavana mstaafu wa Tharaka nithi Onesmus Muthomi Njuki aliyekuwa akizungumza na wanahabari huko diani kaunti ya kwale amesema kwamba ni sharti serikali ya kitaifa na zile za kaunti ziafikie suluhu la kudumu kwa wahudumu hao ili kuhakikisha utoaji wa huduma za afya zinaendelea pasi na pingamizi.
Wahudumu hao waliajiriwa kwa mkataba mwaka 2020 ili kupiga jeki juhudi za wahudumu wa afya nchini kupambana na msambao wa Corona.
BY EDITORIAL DESK