HabariNews

Kaunti Ya Kwale tayari kukabiliana na mkurupuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Wizara ya afya kaunti ya Kwale imeeka mikakati ya kukabiliana na visa vya mikurupuko ya ugonjwa wa kipindupindu ili kuhakikisha usalama wa kiafya katika jamii.

Waziri wa afya kaunti ya Kwale Francis Gwama aliyekuwa akizungumza na wanahabari afisini mwake amethibitisha ufuatilizi wa kesi hizo katika maeneo ya mipakani, hamasa ya kuzingatia usafi miongoni mwa jamii na kutibu maji ya visima na mabwawa ni miongoni mwa mikakati iliyopelekea kaunti ya kwale kukosa visa vya kipindupindu kwa miaka 5 mfululizo.

Hata hivyo amewataka wakaazi kuendelea kuchukua tahadhari na kuhakikisha wana ripoti kesi yeyote inayohusiana na mkurupuko huo ili hatua za haraka zichukuliwe kwa usalama wao wa kiafya.

 

Kadhalka amewataka wakaazi kuendelea kuchukua tahadhari ya mkurupuko huo ili kuepuka maafa yanayotokana na kipindupindu.

Insert …gwama tahadhari