AfyaHabariSiasa

Naibu Gavana Kaunti ya Kwale akanusha madai ya Ukosefu wa maji mji wa Kinango.

Siku moja baada ya wakaazi wa Kinango kuandamana kulalamikia uhaba wa maji naibu  Gavana wa kaunti ya kwale Chirema Kombo amekanusha Madai kuwa mji wa  kinango umekosa bidhaa ya maji Kwa zaidi ya miezi mitano sasa kama ilivyotangazwa na wandamanaji hao.

Chirema aliyekua akizungumza afisini mwake huko matuga amesema kuwa mji wa  Kinango umekosa huduma  za maji Kwa muda wa  siku mbili kutoka Kwa kampuni ya usambazaji maji kwale kwawasco kutokana ukosefu wa ngumu za umeme ulioshuhudiwa katika kipindi cha siku mbili zilizopita.

Vile vile Chirema akiwataka baadhi ya wakazi wa Kinango waliondamana kutoingiza siasa katika suala ya maji na kusema kuwa serikali iko mbioni kuhakikisha wenyeji wa  kwale wanapata maji ya kutosha Kwa matumizi ya kinyumbani na ukulima.
Insert Maji siasa

Tayari huduma za usambazaji maji katika mji WA kinango na viunga vyake zimerejea ikiwemo katika maeneo ya mnadani,Soweto,Timbonina Amani

BY EDITORIAL DESK.