HabariNews

Serikali ya kaunti ya kwale kuanzisha zoezi la kuvisajili vikundi vya VSLA.

Serikali ya kaunti ya kwale kupitia wizara ya huduma kwa jamii na ukuzaji wa talanta inapania kuanzisha zoezi la kuvisajili vikundi vya VSLA na kuvifanya kampuni ili kuviwezesha kufanya zabuni katika serikali na mashirika makubwa.

Waziri katika wizara hiyo Fransisca Kilonzo anasema wizara yake tayari inaendeleza zoezi la kuviunganisha vikundi na wizara ya biashara pamoja na ile ya kilimo ili kuviwezesha vile vikundi ambavyo ni vya bishara kufanya biashara na vile vya ukulima kuendeleza kilimo biashara.

Kilonzo anasema tayari wizara yake imewezesha vikundi zaidi ya 100 kujisajili kama kampuni na wakati wowote kutoka sasa wizara hiyo ikishirikiana na ile ya fedha na biashara watavikusanya vikundi zaidi kote  kaunti ya Kwale ili  kuwapa mafunzo ya kutengenea kampuni na kujiendeleza kibiashara.

Wakati huo huo mama Khadija Changu kutoka kikundi cha INSHAALAH  pamoja na mwenzake Mwanasha Mwachanyuma huko Makongeni Msambweni   ambao pia wamepata mafunzo hayo wanasema wanamatumaini ya kufaidika na tenda  watakaposajiliwa na wakaipongeza serikali kwa hatua hiyo.

Haya yanajiri huku serikali ya Kwale ikiahidi kuinua makundi ya kinamama lengo kuu likiwa waweze kukidhi mahitaji Yao.

BY NEWS DESK