Vikundi 43 vya kilimo, ufugaji na uvuvi ndani ya wadi 20 za kaunti ya Kwale vimekabidhiwa hundi ya shilingi Milioni 109 kama njia mojawapo ya kuenua jamii hizo hali yao ya kiuchumi na pia kimaisha.
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi hundi hizo gavana wa Kwale Fatuma Achani alidokeza kuwa hundi hizo zitaweza kuwasaidia kupambana na athari ya makali ya mabadiliko tabia-nchi kwa kuboresha mazingira ya bahari endapo zitatumika inavyostahili.
Aidha Achani alisema kuwa vikundi 2 vya kilimo,15 vya ufugaji na 24 vya uvuvi ndio watakao faidika na pesa hizo kati yao ikiwa ni pamoja na Tunusuru women group kutoka Munje eneo bunge la Msambweni na Bonje BMU kutoka wadi ya kasemeni eneo bunge la Kinango ambapo vikundi hivi viwili vilipokea shilingi milioni 5 kwa kila kikundi.
Wakati uo huo aliwataka waliopata pesa hizo kuwajibika inavyostahili ili kuepuka kukosa kutimiza malengo ya ufadhili huo uliotolewa na benki kuu ya dunia kupitia shirika la KEMFSED.
BY NEWS DESK