HabariNews

HOSPITALI YA RUFAA YA KAUNTI YA KILIFI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA.


Hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kilifi imepokea msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi na kulinda mazingira wakati wa kutoa huduma kwa wakazi kutoka kwa Aga Khan Development Network.

Vifaa hivyo kama vile mifuko ya kuwekea taka za hospitalini, sabuni, miongoni mwa vifaa vingine, vimetolewa kwa ajili ya kupunguza hatari ya wahudumu wa afya na wagonjwa kupata maambukizi wakati wa matibabu.

Kulingana na waziri wa afya kaunti ya Kilifi Peter Mwarogo vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 2.5 vitasaidia hospitali hiyo kufuata sheria za mamlaka ya kusimamia mazingira nchini NEMA baada ya kutoa huduma kwa wakazi.

Mkuu wa vituo vya kutoa afya nyanjani kutoka hospitali ya Aga Khan Dkt. Sultana Sharman, amesema kupitia mradi huo, katika kipindi cha miezi miwili ijayo wataweka vifaa maalum vya teknolojia ya mawasiliano itakayounganisha hospitali zote kaunti ya Kilifi ili kusaidia wahudumu wa afya kupata mafunzo zaidi.

Mradi wa kupeana vifaa katika hospitali za umekuwa ukifanyika katika kaunti za Mombasa, KIlifi na Kwale.

BY ERICKSON KADZEHA.