Afisa wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Huria, Alex Nziwi amedokeza kuwa sera duni ambazo hazijatilia mkazo jinsi wakaazi wa Kwale wanaweza kunufaika na raslimali waliyonayo zinapelekea wakaazi kutaabika na bidhaa hiyo muhimu jambo alililolitaja kuhujumu haki ya wananchi.
Nziwi amesema kuwa licha ya Kwale kuwa na chemichemi na vyanzo vikuu vya maji ikiwemo Marere, wananchi hawanufaiki na maji.
Afisaa huyo wa Huria amelitaka bunge la kaunti ya Kwale kuja na sheria itakayohakikisha maji kaunti ya Kwale yanawafaidi wakaazi wenyewe badala ya kuuzwa kaunti jirani ya Mombasa.
Ameongeza tayari wanakusanyana sahihi kuhakikisha wanaskuma swala hilo la raslimali ya maji bungeni.
BY EDITORIAL DESK