HabariNews

MAWAKILI WATISHIA KULISHTAKI JOPO LA KUTATHMINI SHERIA NA MUONGOZO WA DINI NCHINI.

Jopo hilo lililoratibiwa kuwa na vikao kumi katika kaunti kumi juma lijalo, limenyoshewa kidole cha lawama kwa kudaiwa kuwa na ubaguzi katika kuendesha vikao hivyo.

Kulingana na mawakili wa mhubiri Ezekiel Odero wa kanisa la New Life International Centre Danstan Omari na Clif Ombeta wamelikosoa jopo hilo kwa kuwanyinya nafasi ya kutoa mapendekezo yao wakati wa vikao vya kutoa maoni vilivyofanyika katika ukumbi wa Juwaba mjini Kilfi huku wakitishia kwenda mahakani kusitisha jopo hilo kufanya kazi yake.

Wakizungumza na wanahabari mawakili hao wanataka vikao hivyo kufanywa katika maabadi  kwani mapendekezo hayo yanahusu viongozi wa dini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jopo hilo Mutava Musimi amewashukuru viongozi wa dini na wakazi kaunti ya Kilifi kwa kujitokeza kwa wingi na kuwa wazi na kuelezea zaidi kuhusu matukio ya shakahola.
Aidha ameeleza kuwa sio watu wote waliopata fursa ya kutoa mapendekezo yao.

Vikao hivyo vinatarajiwa kuendelea leo katika kaunti ya Lamu huku vikao vingine vikifanyika kaunti za Kisumu, Kakamega, Narobi, Tana River, Kwale, Siaya,Migori Homa bay, Kisii na Nyamira.

BY ERICKSON KADZEHA