Wakenya wanaojiuhusisha na michezo ya bahati nasibu wamepata pigo baada ya kuongeza ushuru wa mapato ya michezo hiyo kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 12.5.
Wizara ya fedha ilisema kwamba iliongeza ushuru huo ili kunusuru kuporomoka kwa maadili ya vijana na watoto katika jamii.
Waziri wa fedha Prof, Njuguna Ndung’u alieleza kuwa michezo hiyo ina athari athari mbaya hususan kwa watoto wenye umri mdogo wengine wakiwa bado wangali kuendeleza masomo yao.
“Michezo ya kamari na bahati nasibu ina uraibu mkubwa na inatathiri jamii kwa kiwango kikubwa, hivyo napendekeza bunge serikali iongoze ushuru asilimia 12.5, ili tuwanusuru vijana wetu na hata watoto wa shule wanaoathirika kimasomo,” amesema waziri Ndung’u.
Alizungumza haya alipokuwa akiwailisha Makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, Njuguna amesema hatua hiyo itawakatisha tamaa wale wanaojihusisha na michezo hiyo.