HabariLifestyleNewsSiasa

SERIKALI ITALIPA MADENI YAKE YOTE INAYODAIWA, DENI LICHA YA DENI KUFIKIKA TRILIONI 9.4 KWA SASA, ASEMA WAZIRI WA FEDHA.

Wizara ya fedha imebaini kuwa deni la taifa la Kenya inalodaiwa limevuka kiwango cha shilingi trilioni 9.4 kwa sasa.

Akizungumza wakati wa kusoma makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha 2023/2024 Waziri wa hazina ya fedha na mipango ya uchumi Njuguna Ndung’u amebaini deni hilo linalipika licha ya hali tete ya uchumi kuvurugika kote ulimwenguni.

Hata hivyo Ndung’u amebaini kuwa gharama za kulipa deni hilo zinazidi kuongezeka kutokana na viwango vya juu vya riba na kushukwa thamani kwa shilingi ya Kenya dhidi ya sarafu kubwa duniani.

Licha ya hayo serikali italipa madeni inayodaiwa, wizara ya fedha ikibaini kuwa serikali inanuia kupunguza matumizi yake katika mwaka huu wa kifedha ili kufanikisha ulipaji madeni hayo.

Huku hayo yakijiri Serikali itabuni taasisi maalum ya kutathmini madeni serikali inayodaiwa na wanakandarasi mbalimbali.

Madeni hayo ambayo kufikia sasa ni kima cha shilingi bilioni 537.2 inayodaiwa serikali kuu na shilingi bilioni 157 kwa serikali za kaunti.

Akibainisha hayo wakati wa kusoma bajeti yam waka wa kifedha mwaka 2023/24 waziri wa fedha Prof. Njuguna Ndung’u amesema kuwa madeni ambayo hayajalipwa (pending bills) yamesambaratisha biashara mbalimbali.

Waziri Ndung’u amesema kuwa serikali ikishatathmini na kulipa madeni hayo serikali itaweka sera a kuzitekelza kuhakikisha kuwa kila anayetoa huduma au bidhaa kwa serikali analipwa kwa wakati.