HabariNews

Jamii yahimizwa kukumbatia mbinu mbadala za kutatua mizozo

Jamii imehimizwa kukumbatia mbinu mbadala za kutatua mizozo (Alternative Justice System) ili kudumisha upendo na umoja miongoni mwao.

Akizungumza wakti wa zoezi la kuwaelimisha washikadau wa usalama kuhusu mbinu hizo, Irene Randu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama eneo bunge la Kisauni, amesema kuwa elimu hiyo imewasadia kuelewa kesi wanazostahili kuskiza na kutatua pasi na kukiuka sheria na katiba.

Kulingana na Wycliffe Wathome ambaye ni katibu wa kamati ya AJS katika mahakama ya Shanzu, uamuzi ambao utatolea baada ya mbinu mbadala kutumia lazma unakiliwe.

Maurine Kemtowero ambaye ni wakili amesema lengo la mafunzo hayo ni kuweka viongozi wa kijamii wawe mstari wa mbele katika mambo ya upatanisho na jinsi ya kutoa ushauri kwa jamii.

Kwa upande wake afisa wa shirika la Haki Yetu Julius Wanyama amedokeza kuwa watashirikiana na mahakama kutoa elimu hiyo.

BY JOYCE KELLY