HabariKimataifaLifestyleSiasa

SERIKALI YASEMA HAITAFUNGUA MPAKA WAKE NA SOMALIA KWA SASA.

Waziri wa usalama wa ndani na masuala ya kitaifa Prof. Kithure Kindiki amebaini kuahirishwa kwa shughuli ya ufunguzi wa vituo vya mpaka wake na Somalia kufuatia ongezeko la visa vya ugaidi na uvamizi katika miezi ya hivi karibuni.

Waziri Kindiki amesisistiza umuhimu wa kuupa kipao mbele usalama wa taifa na kusema kuwa serikali imelazimika kuahirisha ufunguzi huo hadi pale mashambulizi ya kigaidi yatatakapodhibitiwa kikamilifu.

 “Serikali ya Kenya na Somalia zimeanza mazungumzo ya kufungua mipaka yetu pande ya Mandera, Kiunga na sehemu zingine mpakani, hatutarudi nyuma kwa huo mpango, lakini kwa sasa kwa mwezi uliopita tumeona hawa wakora wakianza kutatiza amani, tumesimamisha huo utaratibu kidogo tushughulikie hawa magaidi.”

Aidha Waziri Kindiki amesema serikali imebuni sera zinazolenga kuyalinda maslahi ya wakimbizi na jumuiya zinazowahifadhi huku akitoa onyo kali kwa wale wanaotumia nafasi zilizotengewa wakimbizi nchini kutekeleza uhalifu na njama za kigaidi.

Itakumbukwa kuwa vituo vya mipaka ya Kenya na Somalia vilifungwa mnamo mwaka wa 2011 kufuatia msururu wa visa vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa wanamgambo wa Al-shabab.