HabariNewsSiasa

Mahakama kuu yaongeza muda wa kusitisha utekelezwaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023.

Mahakama kuu imeongeza muda wa kusitisha utekelezwaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023 hadi Julai tarehe 10 hii ni kufuataia kesi zilizowasilishwa kupinga sheria hiyo.

Katika kesi hiyo ya kupinga utekelezwaji wa sheria hiyo, Senata wa Busia Okiya Omtatah ameitaka mahakama kumwadhibu mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya kudhibiti kawi na bidhaa za mafuta EPRA, Daniel Kiptoo kwa kukiuka agizo la mahakama la kusitisha utekelezaji wa sheria ya fedha.

Omtatah amemweleza Jaji Mugure Thande kuwa Mkurugenzi huyo alidharau mahakama na kuenda kinyume na agizo la mahakama hiyo kwa kuongeza bei ya mafuta na sasa anastahili kutumikia kifungo cha miezi 6 korokoroni.

Wakati huo huo Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ambaye ni mwakilishi wa mmoja wa waliowasilisha kesi ya kupinga sheria hiyo ametaka swala la ukiukaji wa sheria kushughulikiwa kwanza kabla ya kesi iliyowasilishwa mahakamani kuendelea

Kwa upande wake wakili wa EPRA Prof Gidhu Mwigai amepinga utetezi wa Omtatah na Otiende akishikilia kwamba umekiuka utaratibu wa mahakama kwa kuchelewa kuwasilisha utetezi hivyo kulazimika kubadili baadhi ya maombi kwenye kesi.