HabariNews

Gavana wa Kwale ataka wakaazi kutotozwa ada

Kiongozi huyo amesema kuwa serikali yake inagharamikia matibabu kwa wanaotafuta matibabu katika zahanati  kaunti ya kwale ambapo zoezi zima la kuwasajili wakaazi utafanyika hapo kesho katika baadhi ya vituo vya afya ndani kaunti hiyo.

Achani aliyekuwa ameandamana na Naibu wake Chirema Kombo amewataka wakazi wa Kwale kujiandikisha katika mpango wa Bima ya Afya NHIF ili matibabu yao kugharamikiwa na bima hiyo ya afya.

Hadi kufikia sasa serikali ya kaunti ya kwale chini ya usimamizi wa Gavana Fatuma Achani imeajiri jumla ya wahudumu wa afya 1800 na kujenga zaidi ya Zahanati 165  katika kaunti nzima ya Kwale hii ikiwa mikakati ya kuboresha sekta ya afya Kwale.

BY EDITORIAL DESK