HabariLifestyleSiasa

Wakenya waibua wasiwasi kuhusu gharama ya maisha.

Katika utafiti wa hivi punde wa Kampuni ya InfoTrack asilimia 85 ya wakenya walisema kuna haja serikali kushughulikia kwa dharura suala la gharama ya juu ya maisha.

Fauka ya hayo asilimia 47 ya wakenya inasema kuwa swala la ukosefu wa ajira linafaa kupewa kipaumbele huku asilimia 20 wakilalamikia hadhi ya elimu nchini

Huku hayo yakijiri imeabainika kuwa asilimia 72 ya wakenya inaamini kuwa taifa linaelekea pabaya.

Kwa mujibu wa utafiti wa Infotrack asilimia 12 ya wakenya bado hawajui iwapo taifa lipo pazuri ama pabaya huku asilimia 15 pekee wakiunga mkono uongozi wa Rais William Ruto.

Kulingana na utafiti huo asilimia hiyo ni ongezeko la asilimia 13 kutoka kwa utafiti waliouliofanya mwezi wa Mei mwaka huu.

Gharama ya masha, ukosefu wa ajira na uongozi mbaya ni miongoni kwa sababu zilizopelekea wakenya kusema taifa linaekea pabaya.