HabariLifestyleNews

Azimio kufanya ibada ya maombi ya madhehebu mbalimbali Ijumaa Wiki hii

Mrengo wa Azimio la Umoja umesema maombolezi ya kuwakumbuka watu walioaga dunia yataendela kesho hadi wikendi.

Kinara wa chama cha DAP Kenya chama tanzu katika mrengo wa Azimio, Eugene Wamalwa amesema maombolezo yataendelea Jumamosi kabla ya mwelekeo kutolewa wiki ijayo.

“Tunawapa pole wote walioathiriwa kwa kupoteza wapendwa wao kwa maandamano yaliyotokea, tutasimama pamoja,” akasema Wamalwa

Aidha amesema vigogo wa Azimio watazuru kaunti mbali mbali katika maombolezo yao ili kuomboleza na familia za walioaga dunia walipokuwa wakiandamana.

Kwa mujibu wa Azimio zaidi ya 30 waliaga dunia ambapo asilimia kubwa walifariki kutokana na majeraha ya risasi wakati wa maandamano hayo.

Kwa upande wake kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema muungano huo utafanya maombi ya madhehebu mbali mbali ijumaa hii jijini Nairobi.

Aidha maombi hayo yatafanyika katika kaunti mbali mbali hapa nchini.