Huku Ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya mikoko duniani
Kaunti ya kwale imepiga hatua katika uhifadhi mikoko inayoaminika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Ulimwenguni.
Serikali ya kaunti ya kwale inayoongozwa na Gavana Fatuma Achani hadi kufikia sasa imeongoza shughuli ya upanzi wa zaidi ya mikoko laki 5 kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi kufikia sasa.
Kupitia mradi wa KEMFSED serikali ya kaunti imeongoza shughuli ya upanzi wa mikoko elfu 52 katika eneo la Bonje na mikoko Elfu 50 Huko munje .
Serikali ya kaunti pamoja na wafadhili mbali mbali wamesaidia makundi ya uhifadhi wa mikoko katika uuzaji wa hewa kaa katika mataifa ya ugaibuni yanayohusika katika uchafuzi wa hewa katokana na wingi wa viwanda katika maeneo husika.
Kundi la mikoko pamoja huko Gazi katika eneo la Msambweni wamefanikiwa kuuza hewa kaa kwa dhamani ya shilingi Million 3 huku kundi la uhifadhi wa mikoko huko vanga likiuza hewa kaa ya shilingi Million 6.
Fedha wanazozipata zikielekezwa katika uendelezeshwaji wa miradi ya kijamii ikiwemo ufadhili wa masomo kwa watoto wanaotoka katika jamii maskini pamoja na miradi ya maji katika jamii.
BY EDITORIAL DESK