HabariNews

GSU wakabiliana na wakaazi Nyari-Samburu Kisa Shamba

Watu 8 katika kijiji cha kazamoyo eneo la Taru kaunti ya Kwale wanauguza majeraha katika hospitali ya Samburu baada ya makabiliano makali kati yao na maafisa wa usalama wa kitengo cha GSU. 

Makabiliano hayo yamejiri baada ya wakaazi kufunga barabara ili kusitisha shughuli za mwekezaji mmoja wa kampuni ya makonge huko Nyari kwa madai ya kunyakua kipande chao cha ardhi cha zaidi ya ekari 15.

Wakiongozwa na Emmanuel Mwayaya waliishtumu hatua ya maafisa hao wakisema waliwanyanyasa.

Wakaazi hao wanailaumu serikali wakidai imeshindwa kutatua mzozo huo wa muda mrefu.

Idara ya usalama eneo la Samburu ilithibitisha maafisa 2  wa usalama walipata majeraha madogo madogo  katika kisa hicho   uchunguzi ukianzishwa.

BY EDITORIAL DESK