HabariNews

Uchumi kuimarika, Kampuni ya Naivas Ikizindua Duka lake la 2 Mjini Malindi

Huenda uchumi wa Malindi ukaimarika hata zaidi hivi karibuni kufuatia ufunguzi wa tawi la pili la jumla la Naivas mjini humo.

Kulingana na Afisa Mkuu wa mikakati wa kampuni ya Naivas nchini Andreas Von Paleske, tawi hilo ni la pili mjini Malindi na la 97 kote nchini.

Afisa huyo amebaini kuwa kampuni hiyo inalenga kufikia matawi 100 ifikapo mwisho wa mwaka huu na hivyo kubuni nafasi zaidi za ajira kwa vijana nchini.

“Kufungua kwa duka letu la 2 hapa Malindi kuna maana kubwa sana kwetu, kufungua tawi hili ni kutokana na kukua kwa biashara zaidi baada ya tawi la kwanza miaka kadhaa iliyopita. Sababu kubwa ya kwanza ni kufungua nafasi za ajira kwa wakazi wa hap ana Pwani, tuna matawi 10 Pwani na tunanuia kufungua maduka mengi zaidi,” akasema Bw. Paleske.

Katika taarifa yake msimamizi wa jumba la Festival Mall linalohifadhi tawi la pili mjini Malindi Mwendwa Thuranira amebaini kuwa kunazo nafasi zaidi za wafanyabiashara wadogo wadogo ndani ya jumba hilo.

Thuranira amewarai wawekezaji kujitokeza ili kuwekeza katika mji huo wa kitalii akisema kuwa kwa sasa usalama umeimarika eneo hilo.

“Kama managers wa mall hii tunawasihi wanabiashara wote wadogo pia waje kufungua biashara zao hapa. Bado kuna nafasi zimebakia, ukiwa karibu wafanyabiashara wakubwa ‘ma giant’ kama Naivasa wewe pia utakua Mkubwa na ‘giant’ kibiashara.

Kauli yao inajiri huku utafiti ukionesha kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vijana kote nchini haina ajira hivyo kupelekea wengi wao kuhangaika na hata baadhi yao wakigeukia kujihusisha na visa vya uhalifu.

BY EDITORIAL DESK