Afya

Uhaba wa Dawa Hospitali za Umma, faida kwa Wamiliki wa Maduka ya Dawa Kilifi

Serikali ya kaunti ya Kilifi imetakiwa kuboresha huduma za afya katika hospitali za umma hasa maeneo ya mashinani.

Baadhi ya wakaazi katika wadi ya Ruruma kaunti ya Kilifi wamedai  kuwa mara nyingi wanapofika katika hospitali hizo wamekuwa wakikosa matibabu yanayofaa kutokana na uhaba wa dawa.

Kulingana na wakaazi hao wakiongozwa Nuru Kobe, serikali ya kaunti imetelekeza ya msingi kwa wananchi hususan wale wanaoishi mashinani.

“Zile dawa nazo wanakupewa hata dawa moja yenyewe, dawa moja itakusaidia na nini? Hiyo dawa moja haitakusaidia lolote au hata uandikiwe ukanunue ukanunue, huku mashinani kuna pesa?” Nuru alihoji.

Vile vile, wamekemea vikali hatua ya baadhi ya wahudumu wa afya katika taasisi hizo kwa kile wanachokitaja kama kuwadharau watu wanaotafuta huduma za afya.

Wamesema hatua hiyo ni miongoni mwa sababu nyingi zinazowafanya kususia hospitali za uma na badala yake kutafuta huduma za afya katika maduka mbalimbali ya kuuza dawa pamoja na kwenye hospitali za kibinafsi.

“Waeza kwenda pale una shida yako alafu wanakwambia kaa hapo mwanzo uningojee mimi niko na kazi au nimechoka. Nimekwenda kuviona mwenyewe hasa, keti pale uningoje wala au njoo kesho, sasa nikija kesho hivi sasa nitafanyaje? Ndio maana twaenda madukani twanunua madawa, mtu unakula na hutaskia vizuri.” Aliongeza mkaazi mwingine.

BY EDITORIAL DESK