HabariNews

Gavana wa Kilifi afanyia mageuzi Baraza lake la Mawaziri

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro amefanya mabadiliko kwenye mawaziri wake kufuatia kifo cha Afisa Mkuu na Waziri wa uchumi Samawati katika kaunti hiyo Rahab Karisa aliyedaiwa kuuawa na mwajiri wake wiki iliyopita.

Gavana huyo amemteua Habat George Mwachiro ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa mazingira na usimamizi wa taka kuwa kaimu Afisa Mkuu wa uchumi Samawati.

Raymond Ngala ambaye alikuwa Waziri wa Utalii Biashara na Maendeleo amehamishwa hadi Wizara ya Fedha na Mipangilio huku Yahya Shoshi akiwa wa Utumishi wa Umma.

Naye Clara Chonga alihamishwa kutoka kwa Wizara ya Elimu hadi ya Biashara huku nafasi yake ikichukuliwa na Frankline Kaingu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ugatuzi na Utumishi wa Umma.

BY EDITORIAL DESK