Naibu kiongozi wa chama cha PAA Hassan Albeity amesema Rais William Ruto ana nafasi kubwa kubadili uongozi wa taifa kutokana na imani wakenya waliyonayo kwake na hadhi yake kama kiongozi.
Albeity amesema rais Ruto hana imani ya kufanya handshake na mrengo wa upinzani bali mapatano na mrengo huo kwa minajili ya kuendeleza sera za taifa.
Ameongeza kuwa iwapo kutakuwa na handshake mamlaka ya naibu wa Rais Rigathi Gachagua huenda yakapungua.
Pia Albeity ameongeza kuwa ni sharti kuwe na upinzani wenye Nguvu ili kuangazia maovu yanayotendeka nchini ikiwepo kumaliza ufisadi huku akisistiza haja ya kuwepo ofisi ya mkuu wa upinzani katika bunge ili kufuatilia yanayoendelea nchini.
Wakati huo huo amepongeza hatua ya Rais William Ruto kutoa mbegu kwa wakulima akisema hatua hiyo itaweza kukabiliana na baa la njaa akihimiza wakulima kuhifadhi mahindi yao badala ya kuyauza kwa bei rahisi.
BY EDITORIAL DESK