HabariNews

Vyeo Vya Mawaziri Nchini Kenya ni Vya Kisiasa?

Mwanasheria kutoka shirika la MUHURI Omar Elmawi amesema nafasi za mawaziri humu nchini zimekuwa zikitumika kisiasa na viongozi walio mamlakani.

Akiongea na meza yetu ya habari Wakili huyu msomi Bw. Elmaawi alisema mara nyingi viongozi huchukua manufaa kwa wale ambao waliwaunga mkono wakati wa kampeni zao na kusahau Mkenya aliyempigia kura.

“Ukiangalia mwanzoni mwa serikali zetu nafasi hizi wanazichukua kama kuwapatia manufaa wale watu ambao waliwatafutia kura ili waweze kuingia mamlakni ukiangali uongozi wa Rais Ruto mawaziri wenye walichaguliwa ambazo zilikuwa kortini ikiwemo za mauaji.” Amesema Elmawi.

Alisema ni sharti mawaziri wanapochaguliwa kuwe na taarifa kamili za anayechaguliwa akitolea mfano ya baadhi ya mawaziri Waliochaguliwa licha ya kuwa na kesi mbali mbali.

“Nafasi hizi zinahitaji mtu tunayemchagua ni mtu ambaye hatuna wasiwasi wowote kumhusu ikija kwenye maswala kwamba ni watu wazuri na kwamba hawataleta matatizo kawaida lazima uwe umefanya background check na kuwaangalia je kuna kesi zinawahusu, je, wamekuwa wakizembea kazini kwao?” Alikariri.

Wakili huyu msomi aliongeza kuwa kuna haja ya mawaziri hao kubadilishwa iwapo watakuwa hawatekelezi majukumu yao waliyochaguliwa katika wizara tofauti tofauti akisema kuendelea kuhudumu kwenye wizara hizo ni kupoteza mali ya umma bila mafanikio.

“Mawaziri ni watu ambao wanalipwa pesa nyingi ambazo zinatoka kwenye kodi ya wanainchi na ni huzuni kubwa kuona tunalipa watu ambao wamezembea kwenye kazi yao mwisho wa siku tunataka kuona kazi yao sio kusimama mbele ya mikutano ya kisiasa lakini watupe taswira yao na mipango yao.”

Elmaawy amedokeza kuwa itakuwa bora zaidi iwapo mawaziri watachaguliwa kulingana na tajriba walizosomea kama njia moja ya kufanya mabadiliko katika wizara zao na kuchangia katika ukuaji wa taifa.

BY EDITORIAL DESK