Umoja wa Afrika (AU) ulisimamisha shughuli zake zote Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi uliopita.
Baraza la Amani na Usalama la AU lilitoa wito kwa nchi zote wanachama wake na jumuiya ya kimataifa kujiepusha na hatua zozote zinazoweza kuhalalisha utawala wa kijeshi nchini Niger.
Ulikariri wito kwa viongozi wa mapinduzi kumwachilia huru Rais mteule Mohamed Bazoum.
Jumuiya ya Uchumi wa Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS tayari imetishia hatua za kijeshi kumrejesha kazini.
Serikali ya Niger imesema kuwa utawala wa kiraia hauwezi kurejeshwa mpaka baada ya miaka mitatu, lakini hili limepuuzwa na ECOWAS kuwa halikubaliki.