HabariMombasaNews

Serikali kutoza Ada maradufu kwa waagizaji madini na samaki Nje

Serikali itawatoza ada wafanyabiashara wa viwanda wanaoagiza kemikali maalum ya Klinka inayotumika kutengenezea saruji kutoka mataifa ya nje.

Waziri wa madini, Uvuvi na Uchumi Samawati Salim Mvurya alibaini kuwa bidhaa hiyo inaweza kutengenezwa hapa nchini na wenye viwanda aidha wanaweza hata kutumia bidhaa ya gypsum na nyinginezo kutengenezea madini ya saruji.

“Hatuoni haja ya kwamba watu waweze kuleta clinka kutoka ng’ambo wakati sisi hapa tuko na limestone, tuko na gypsum kwa hiyo ndio maana tumeweka gharama kidogo ya wale wanao import viwanda vya hapa Kenya viweze kufanya value addition na kubuni nafasi za kazi,” alisema Mvurya.

Kulingana na Mvurya, serikali inataweka ada kwa kutoza ushuru kwa waagizaji wa samaki kutoka mataifa ya nje ili kuongeza mapato nchini sawia na kuimarisha biashara ya samaki kutoka hapa nchini.

“Tutaweka levy hapo kidogo kwa uagizaji wa samaki kutoka nje ili tuhakikishe tunaongeza mapato na kazi hapa nyumbani,” alisema.

Hatua hiyo inatarajiwa kusaidia kuimarisha sekta ya madini na viwanda nchini sawia na kubuni nafasi za ajira.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria hafla moja mjini Mombasa Waziri Mvurya alisema kuwa serikali itaweka ada kwa kutoza ushuru  waagizaji wa samaki kutoka mataifa ya nje ili kuongeza mapato nchini sawia na kuimarisha biashara ya samaki wa kutoka hapa nchini.

BY EDITORIAL DESK