HabariNews

‘La! Si asilimia 4 pekee,’ Gavana Abdulswamad Sharrif Nassir Akosolewa

Wadau katika sekta ya utalii wakosoa kauli ya Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir kusema kuwa ni asilimia 4 pekee ya mapato ya kaunti hiyo yanatokana na sekta ya utalii.

Mkurugenzi wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli za Kitalii Pwani, Sam Ikwaye alisema kuwa sekta ya utalii ni miongoni mwa sekta zinazochangia mapato makubwa humu nchini na huenda takwimu zilizotolewa na gavana Nassir zisiwe za ukweli hadi pale zitakapochunguzwa kwa makini.

Gavana Nassir alibaini kuwa  kukosekana kwa mfumo wa anga huru (Open sky policy) ndiko kulichangia pakubwa kushuka kwa mapato hadi asilimia 4.

Ikwaye aidha alikosoa kauli hio akisema kuwa serikali ya kaunti ilikosa kuelewa mchango wa sekta hiyo jambo ambalo alilolitaja kuchangia kudorora kwa hamu na ari ya uwekezaji katika sekta hiyo.

“Sekta ya utalii Kenya nzima ni sekta ambayo imekuwa inafanya vizuri sana na ikumbukwe uwekezaji mwingi unapatikana eneo la Pwani na hivyo labda zile takwimu ambazo Gavana alizitoa zinahitaji kuweza kuchunguzwa tena na kuhakikishwa.” Alisema Ikwaye

Kaunti ya Mombasa inasifa ya kupokea wageni kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni kutokana migahawa, vitutio pamoja na mandhari  na fuo za kupendeza.

Hata hivyo Abdul Majid Igombo Mkuu wa kitengo cha maswala ya kijamii Fort Jesus alisemakuwa mwaka huu sekta ya utalii ilitiafora ikilinganishwa na mwaka jana kwa kuzingatia idadi ya wegeni wanaoingia nchini.

Kauli ilikosa kuwiana na matamshi ya Gavana Nassir, Igombo Akibaini kuwa kaunti ya Mombasa inapokea watalii wengi kutoka maeneo tofauti tofauti hapa nchini na kutoka mataifa ya nje.

“Kulingana na kauli ya Gavana sioni kama alivyozungumza ni kweli, kwa sababu utalii mwaka huu umefana sana ikilinganishwa na mwaka jana kutokana na idadi ya wageni ambao wamekuja, sijui ametoa wapi takwimu hizo lakini  asilimia 4 ni kidogo sana.”Alisema Igombo.

Wakati uo huo Igombo alipongeza hatua ya kufunguliwa kwa anga huru ya Mombasa-Open Sky Policy akisema kuwa hatua hiyo ni mwamko wa kuendeleza kupiga jeki zaidi sekta ya utalii ukanda wa Pwani na nchi kwa jumla.

BY EDITORIAL DESK