HabariNews

Miti Asili hatarini na kutatiza Azma ya pandaji Miti nchini.

Juhudi za kupanda miti na kufikia bilioni 15 azma ya serikali ifikapo mwaka 2030 hapa nchini, zimekumbwa na changamoto kufuatia miti ya asili kuendelea kukatwa maeneo tofauti tofauti humu nchini. Changamoto hizo zimepelekea mashirika ya kijamii kaunti ya Kilifi kuitaka serikali kutekeleza sheria ya kutunza miti hiyo asili.

Mshauri wa uongozi na sheria kaunti ya Kilifi Kelly Robert Banda, aliitaka serikali kuhimiza utekelezwaji wa sheria za utunzaji wa miti asili pamoja na sheria zilizopo kuhusu maswala ya tabia nchi ili kukabiliana na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kulingana na Banda, wananchi wanakosa hamasa ya kutosha kuhusu sheria zinazoambatana na mabadiliko ya tabia nchi kumechangia wengi kutowajibika ipasavyo katika kukabilianana athari hizo.

“Ukiangalia ile wajibu wa rais ya kuwa tupande 15 billion trees, kweli tutatimiza kama huku kwengine tunakata na tunapata bidhaa ya miti ya Mibuyu zinasafairishwa. Tusipohifadhi miti hii ya asili kizazi kijacho kitafanya kusoma kwa vitabu kuwa miti hii ilikuwepo, ni wakati sasa serikali kuu na hata ya Kilifi ione kuwa kulipa muhimu suala hili na umuhimu wa miti hii. Kilifi kaunti iweke kipaumbele kwa masuala ya miti na kuhakikisha kuwa sera ama policy hizi zinatekelezwa ili tuifadhi asili yetu,” alisema

Rais wa vijana kaunti ya Kilifi Asumptha Mbeyu aliitaka serikali ya kaunti kutoa njia mbadala kwa wakazi wanaotegemea biashara za miti kujitafutia riziki ili kuhakikisha kwamba lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi linafanikishwa na kila mmoja.

Hata hivyo Mbeyu alihimiza kuchukuliwa kwa uzito swala la uhamasishaji wa wakazi katika utekelezwaji wa sheria zinazowahusisha vijana katika maswala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“imefikia mahali hata kama vijana tukijaribu kuongea kuhusianana ukataji wa miti tunaambiwa kama serikali yenu imekubali mibuyu itolewe na ipelekwe nchi nyingine ni kumaanisha kwamba hawajali miti kwasababu kuna mahali ambapo sharia hakuna ama zile ambapo ziko ni arts. hazina policy bado . lakini hapa kwetu kilifi kaunti tumeweka kipao mbele arts. na tumesahau policy kuimpliment hio policy inakua ni ngumu kwetu”  alisema Mbeyu.

Taifa la Kenya linatarajia kuandaa kongamano la kuangazia maswala ya tabia nchi barani Afrika mapema mwezi Septemba mwaka 2023.

BY ERIKSON KAZEHA