HabariNewsScience

KEMRI yaandaa Kongamano kujadili Mabadiliko ya Tabianchi

Watafiti kutoka KEMRI na wadau wengine kwenye sekta ya afya waliandaa kongamano la pili la afya na athari za mabadiliko ya tabianchi Agosti 28, 20203.

Ukataji miti,uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na hewa chafu ni moja wapo ya changamoto kubwa zinayochangia katika mabadiliko ya tabia nchi.

Haya ni kulingana na ELIJAH SONGOK, mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa matibabu nchini (KEMRI).

Watafiti kutoka KEMRI aidha, wametaja athari mbalimbali za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo magonjwa na uharibifu wa hewa.

Elijah alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuweka baadhi ya mikakati itakayoweza kutatua matatizo yanayosababisha mabadiliko ya tabianchi.

 

BY EDITORIAL DESK