HabariNews

Maseneta Wateta katika Bunge la Seneti, Cherargei akifurushwa Nje

Kizaazaa kilizuka katika Bunge la Seneti wakati wa mjadala wa kuidhinisha kamati ya mazungumzo ya maridhiano.

Kizaazaa hicho kilijiri kati Seneta wa Nandi Samson Cherargei aliyekiuka maagizo ya Spika akilalamikia kuitwa mtoto mdogo na seneta wa Kilifi Stewart Madzayo.

Spika wa bunge la seneti Amason Jeffa Kingi alilazimika kumfurusha bungeni Cherargei kwa siku nzima baada ya seneta huyo kudinda kumsikiliza.

Seneta Cherargei tafadhali keti chini, Senata Cherargei keti chini! Senator Cherargei you take your seat or I order you to leave the chambers……Senator Cherargei you’re out of order kindly proceed to leave the chambers! Sergent at Arms! Escort the member out of the chamber,” alisema Spika Kingi.

Baadaye Kingi, alimtaka Seneta Madzayo kumwomba msamaha Cherargei kutokana na kauli aliyomtamkia. Hatua iliyombidi Seneta Madzayo kusalim amri.

Kikao hicho cha Jumanne, Agosti 29 kilitumika kuidhinisha kubuniwa rasmi kwa kamati ya mazungumzo ya kiufundi yenye watu wanane.

Hatua hii inamaanisha kwamba kamati hizo mbili ambazo tayari zimebuniwa na wanachama kuteuliwa, zitaanza majukumu yake rasmi siku ya Jumatano (Agosti 30, 2023) ikiambatana na makubaliano yaliyowekwa baina ya pande za Kenya Kwanza na Azimio la Umoja.

BY EDITORIAL DESK