HabariNews

Mhame Kenya, muishie Gerezani au muende mbinguni! Ruto azidi kuwaonya Mafisadi

Kwa mara nyingine tena Rais William Ruto ameshikilia msimamo wa kupambana na ufisadi kikamilifu ili kuhakikisha mali ya umma yanalindwa dhidi ya uporaji na watu binafsi nchini.

Akizungumza baada ya kufanya kikao na Baraza la Mawaziri Ruto alitoa onyo kwa mafisadi kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria ikiwemo kusukumwa gerezani au hata kulazimika kuhamia mataifa mengine.

“mtu yeyote ambaye anapanga ati kuiba pesa ya serikali, wezi wote, matapeli hawa watu mambo yao ni tatu, aidha wahame kenya ama waende jela ama waende mbinguni hakuna dawa ingine” Alisema.

Kulingana na Ruto, serikali yake kamwe haiwezi kuwavumilia mafisadi wakiendelea kufuja mali ya umma.

Ruto aidha kuwa alisema ni lazima pesa zilizotengwa na serikali kwa ajili ya kufanikisha miradi ya maendeleo mashinani zimfaidi mwananchi badala ya kuishia mifukoni mwa watu.

BY EDITORIAL DESK