HabariNews

Zaidi ya vijana 350 wamefuzu baada ya kufaidika na elimu ya maswala ya teknolojia Katika kaunti ya kilifi

Zaidi ya vijana 350 wamefuzu baada ya kufaidika na elimu ya maswala ya teknolojia Katika kaunti ya kilifi. Mpango huo uliwashirikisha shirika la power learn project na serikali ya kaunti ya kilifi kwa lengo la kuwapa vijana kaunti hiyo elimu ya kidigitali na maswala nzima ya teknolojia kwa kiasi kikubwa ili waweze kujipa ajira sambamba na kuwawezesha kuajiriwa katika sekta tofauti tofauti humu nchini na hata ughaibuni.

Serikali ya kaunti ya kilifi kupitia naibu gavana Flora chibule amesema kuwa tayari robo ya waliofuzu watapewa ajira kaunti hiyo.

Baadhi ya mahafala wamedokeza kuwa wamefaidika na elimu hiyo huku wakipongeza hatua ya serikali ya kaunti Hiyo kuwapa nafasi ya kuwawezesha na kunufaika na ujuzi wa teknolojia sambamba na maswala muhimu ya kidigitali.

BY NEWS DESK