GamingHabariMichezoNewsSports

Sajili za lala salama Kuwasha Moto wa EPL Uingereza

Timu mbalimbali barani ulaya zilijitosa sokoni dakika za lala salama kufanya usajili ili kuimarisha vikosi vyao tayari kwa msimu wa 2023/2024 ambao ulianza rasmi  kwa kishindo Agosti 11, 2023.

Mancher City imekuwa timu ya mwisho kufanya ndani ya Uingereza kwa kutoa kiima cha pauni milioni 47.7 kunasa huduma za Mreno Matheus Nunes kutoka wolveshampton.

Chelsea Vile vile Haikusalia Mkiani, wanasamawati hao walimnasa Kinda Kutoka Manchester City Cole Palmer kwa dau la pauni milioni 40 huku timu ya Brighton nayo imemnasa chipukizi Ansu Fati kutoka FC Barcelona kwa mkopo.

Sajili hizi zinatarajiwa kuimarisha viwango vya soka ndani ya ligi kuu ya Uingereza. Kila timu ikiwa ,bioni kujinoa nakuziba pengo katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa wa ligi hio.

Hata hivyo AS Monaco ya Ufaransa ilimsajili Folarin Balogun kutoka kutoka arsenal kwa pauni milioni 34. Balogun alitia sahihi kandarasi ya miaka mitano na miamba hao wa ligi 1, ufaransa.

BY EDITORIAL DESK