Mashirika yasio ya kiserikali yaliopanga mkutano wa kujadili mustakabali wa maswala ya ardhi na ujenzi wa nyumba za bei nafuu kaunti ya Mombasa yamempa waziri wa ardhi na mipangalio ya mji, mohammed Hussein AMADO, muda wa wiki 2 kujibu maswali ya wananchi la sivyo yataanda maandamano kuonyesha kutoridhishwa na uongozi wa waziri huyo.
Mwenyekiti ukanda wa pwani Zedekia adika pamoja na viongozi wa mashirika hayo hawakuridhishwa na hatua ya waziri huyo kutohudhiria kikao kilichoratibiwa kujadili mambo kadha yanayawathiri wakazi wa Mombasa.
Adika aidha, alimtaka waziri huyo kuweka bayana maswala ya kisheria kuhusiana na miradi ya ujenzi wa nyumba wanazohisi kuwa zimekosa kufuata taratibu za kisheria.
Licha ya waziri huyo kutofika , mwakilishi wake Abdul aziz, mhandisi katika idara ya ujenzi wa nyumba kaunti ya Mombasa, alijipata pabaya baada ya wakazi waliohudhiria kikao hicho kudinda kumpa maskio kujibu maswali kabla ya mwenyekiti huyo kuingilia kati na kutuliza joto hilo.
Wakili Adika alitaja ushirikiano wao kama mashirika na wakazi kutuma maswali katika ofisi ya waziri huyu na kutaka majibu baada ya siku 7 la sivyo wataandamana hadi ofisini mwake.
Kwa upande mwingine kina mama wakiongozwa na Grace Oloo kutoka shirika la ujamaa, hawakupendezwa na hatua ya waziri huyo wakisema kuwa muktano ulipangwa chini ya mwezi mmoja na waziri alikuwa na taarifa ya kutosha
Oloo alipaza kilio cha lawama wazopitia kina mama kutokana na ujenzi wa nyumba hizo.
Hata hivyo baadhi ya washikadau walipaza malalamiko yao ya kutoridhishwa na uamuzi wa kuweka afisi za ardhi katika majengo ya bima towers horofa ya sita hatua wanayodai kulemeza juhudi za wazee pamoja na jamii zinazoishi na ulemavu kufikia huduma hizo.