Rais William Ruto alifungua rasmi kongamano la Bara Afrika kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Septemba 4, 2023 katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi.
Ruto katika hotuba yake alitangaza kuweka mikakati ya kufutilia mbali stakabadhi za visa kwa waafrika wanaoingia kiziara katika taifa la Kenya.
Ruto alisema kuwa serikali yake inapanga kufutilia stakabadhi hizo zinazohitajika kuingia nchini akitaja kuwa Kenya ni nyumbani kwa kila mmoja kutoka bara la Afrika.
“Nirudusu niwakaribishe nyumbani. Miezi isiyo mbali kutoka sasa, tutaondoa hitaji la visa kwa Waafrika wanaotembea Kenya. Si haki unapotembea nyumbani unaagizwa kuwa na visa, Si haki kwa Mwafrika kuagizwa visa anapotembea nyumbani” Alisema
Hatua hiyo ya kufungua mipaka ya Kenya kwa nchi zote za Bara Afrika, inawiana na mikakati ya Afrika Mashariki ambapo raia wa ukanda huu hawahitaji kuwa na visa kuzuru nchi yoyote Afrika Mashariki.
Kwa upande mwingine Dkt Ruto alihimiza wadau hasa kutoka bara la afrika kukumbatia nishati mbadala, kuliko kutegemea umeme akidai kuwa bara hilo lina rasimali za kutosha.
Ruto hata hivyo ameelezea umuhimu wa afrika kukumbatia mikakati ya kufanikisha kilimo cha kuboresha mazingira.
“ Takriban waafrika milioni 600 wanakosa nguvu za umeme, wengine milioni 150 wanapigania nishati zisizotegemewa na karibu watu bilioni moja wanakosa kufikia ya nishati safi ya kupikia. Tuko na uwezo wa kutoa nishati ya kutegemewa kwa waafrika kote barani kwa jumla kufikia mwaka 2030”
Kuhusu maswala ya mabadiliko ya hali anga rais ruto amesema kuwa kongamano hilo la kwanza katika bara la afrika ni mwamko mpya kwa waafrika.
“Niko na Imani kuwa kuanzia sasa kuenda mbele, tuko nakila kinachohitajika kutengeneza matokeo yatakayonufaisha pande zote kutokana na mazungumzo haya ya mabadiliko ya anga”
Takribani viongozi wakuu 20 Barani Afrika wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo linalolenga kuangazia changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi na jinsi ya kudhibiti hali hiyo.
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni kuendeshwa kwa ukuaji wa mazingira na suluhu ya fedha za hali ya anga Afrika na duniani kote.